Wazo hili lilibuniwa wakati wa enzi ya Profesa Wilfred H.Whitely, ambaye wakati huo alikuwa ndiye Mkurugenzi wa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili, ikiwa ni miaka 25 baada ya kuchapishwa kwa kamusi ya Johnson ijulikanayo kama Standard Swahili-English Dictionary (1939). Wazo la kutunga kamusi hii ilianzishwa mwaka 1964 na Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili (ambacho kuanzia mwaka 1972 kilijulikana kama Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili).
DIBAJI YA TOLEO LA KWANZA LA KAMUSI YA KISWAHILI-KIINGEREZA Kamusi hii ya Kiswahili-Kiingereza ina historia ndefu.